Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la AFP limemnukuuu Bi Annalena Baerbock akisema hayo na kuongeza kuwa, wakati nchi fulani inapowekewa vikwazo, inabidi kuweko mikakati ya kuendeleza vikwazo hivyo kwa muda mrefu. Lakini kuiwekea vikwazo nchi kwa muda wa wiki tatu na baadae tugundue kuwa hatuwezi kuendelea na vikwazo hivyo, ni jambo lisilo na maana hata kidogo.
Amesema, iwapo Ujerumani itazuia kuingia nchini humo mafuta, gesi na makaa ya mawe kutoka Russia na baada ya kupita siku chache igundulike kuwa umeme umekatika nchini Ujerumani, sisi wenyewe tutalazimika kutia ulimi puani na kuondoa wenyewe vikwazo hivyo.
Kabla ya hapo pia, Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ujerumani aliwahi kuiambia televisheni ya ZDF kwamba, sisi tuko tayari kutoa pigo kubwa la kiuchumi na kifedha kwa Russia kutokana na hatua yake ya kuishambulia kijeshi Ukraine, lakini kama leo na kesho Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya zitakosa umeme, tutaweza kweli kuzuia vifaru vya Russia.
Hivi sasa Ujerumani inadhamini asilimia 55 ya gesi na asilimia 42 ya mafuta na makaa ya mawe kutoka Russia na kama itaacha kidogo tu kutumia gesi, mafuta na makaa ya mawe ya Russia, uchumi wa Ujerumani utasambaratika.
Ujerumani si nchi pekee ya Ulaya inayopinga vikwazo vya kiuchumi na kifedha kwa Russia. Kwa miaka mingi sasa nchi za Ulaya zinajaribu kutokuwa tegemezi kwa nishati ya Russia lakini hadi hivi sasa zimeshindwa. Karibu asilimia 40 ya gesi inayotumiwa na nchi za Ulaya inatokea Russia.
342/